APK rasmi kutoka Codeblock Limited
Pakua Drafti Ligi kwa Android
Faili rasmi la APK, moja kwa moja kutoka kwetu. Akaunti yako itaendelea hata ukihamia toleo la Google Play baadaye.
- Toleo
- 0.1.1
- Ukubwa
- 65.8 MB
- SHA-256
- 42e7db5a22a40c3442d211bc287eb16511e46997c4f877aabefdcc1bc02fd5b4
Jinsi ya kusakinisha
-
01
Pakua faili
Gusa Pakua APK. Kivinjari kikiuliza kama unataka kuhifadhi faili, chagua Pakua.
-
02
Ruhusu usakinishaji
Fungua faili. Ukiulizwa, gusa Mipangilio na uwashe “Ruhusu kutoka chanzo hiki” kwa kivinjari chako (kwa mfano Chrome) au programu ya Faili. Kwenye simu za zamani: Mipangilio › Usalama › Vyanzo visivyojulikana.
-
03
Sakinisha na ufungue
Gusa Sakinisha, kisha Fungua. Ingia kwa namba yako ya simu.
-
04
Zima ruhusa tena (hiari)
Ukimaliza, nenda Mipangilio › Programu › Ufikiaji maalum › Sakinisha programu zisizojulikana, na uzime ruhusa uliyowasha.
Kuhusu Google Play Protect
Kwa sababu APK haitoki Google Play, Play Protect inaweza kuonyesha onyo au kuomba kuichunguza programu. Chagua “Chunguza programu”, au “Maelezo zaidi › Sakinisha hata hivyo”.
Pakua APK kutoka drafti.co.tz pekee, kamwe si kutoka magrupu ya WhatsApp au tovuti nyingine. Hatutakuomba msimbo wako wa kuingia.
Hakiki faili
Kwa wanaotaka uhakika zaidi: SHA-256 ya faili ulilopakua lazima ilingane na iliyo hapo juu.
# macOS / Linux shasum -a 256 drafti-ligi.apk # Windows certutil -hashfile drafti-ligi.apk SHA256
Masasisho
Programu itakujulisha toleo jipya likitoka. Pakua tena kutoka ukurasa huu na usakinishe juu ya lililopo: akaunti, almasi na skini zako zinabaki.
Una iPhone?
Drafti Ligi inakuja kwenye App Store. Tutaweka kiungo hapa ikiwa tayari.