Ruka hadi maudhui

89 mechi leo

Drafti ya Kitanzania. Sasa mtandaoni.

Cheza na watu wa Tanzania na duniani kote kwa sheria za Kitanzania: mfalme anaruka, kula ni lazima, njia ni yako.

Mechi zenye viwango · Bullet, blitz na rapid · Msimamo wa taifa

Sheria

Sheria halisi za Tanzania.

Si mchezo wa kigeni uliobadilishwa jina. Mchezo unasimamia kila hatua, kama vijiweni.

  1. 1 Askari husonga na kula mbele tu
  2. 2 Mfalme anaruka umbali wowote
  3. 3 Kula ni lazima, njia ni yako
  4. 4 Askari akivishwa taji katikati ya kula, zamu inaishia hapo
Anza mchezo wako wa kwanza

Ligi

Cheza ligi. Panda daraja.

Anzisha klabu ya mtaa, chuo au ofisi. Kila wiki klabu yako inakutana na nyingine, na nahodha anapanga safu.

8
wiki kwa msimu
4–6
bao kwa mechi ya klabu
20%
wanapanda, 20% wanashuka
Jiunge na ligi

Skini

Ubao wako, mtindo wako.

Usiku, mbao ya Mninga na mkusanyiko wa Mashabiki. Unabadilisha bao na vipande; sheria ni zilezile.

  • Usiku
  • Classic Mninga
  • Mnyama
  • Wananchi
  • Lambalamba

Miundo iliyochochewa na mashabiki. Haihusiani na, wala haijaidhinishwa na, klabu yoyote. Kuhusu mkusanyiko wa Mashabiki

Chagua mtindo wako

Mubashara

Tazama mubashara. Piga soga.

Fainali za arena, swiss na mtoano, saa zikienda. Mechi za ushindani zinaonyeshwa nusu-hatua mbili nyuma, na wachezaji hawaoni soga hadi mechi iishe.

Soga inachujwa: matusi, viungo na namba za simu huzuiwa.

Tazama fainali ijayo

Bao liko tayari. Zamu yako.

Pakua Drafti Ligi, pata kiwango chako na upande msimamo.

Kwa biashara

Una swali la kibiashara? Wasiliana nasi.

Tuandikie · support@codeblock.co.tz

Maswali

Maswali ya mara kwa mara

Maswali zaidi? Tembelea ukurasa wa Msaada
Viwango vinafanyaje kazi?

Kila mechi yenye viwango inapandisha au kushusha kiwango chako, kando kwa bullet, blitz na rapid. Unakutanishwa na wachezaji wa kiwango chako, na msimamo unaonyesha nafasi yako kitaifa, kimkoa na kwenye klabu yako.

Mnatumia sheria zipi?

Drafti ya Kitanzania: bao la 8×8, askari wanasonga na kula mbele tu, mfalme anaruka umbali wowote, na kula ni lazima lakini unachagua njia. Askari akifika mwisho katikati ya kula, zamu inaishia hapo.

Mnawashughulikiaje wanaodanganya?

Kila mechi yenye viwango inakaguliwa na mfumo wetu wa mchezo wa haki. Udanganyifu ukithibitishwa, mchezaji anaadhibiwa na mabadiliko ya viwango ya mechi hizo yanarudishwa.

Programu iko Google Play na App Store?

Ndiyo, tafuta Drafti Ligi kwenye Google Play au App Store. Pakua

Napataje almasi?

Ndani ya programu kupitia Google Play au App Store. Ukiwa Tanzania, pia kwenye tovuti hii kwa M-Pesa, Mixx, Airtel Money au HaloPesa. Sarafu unazipata kwa kucheza. Almasi zinabadilisha mwonekano wa bao lako tu, si uwezo wako mchezoni.

Wachezaji wengine wanaona namba yangu ya simu au barua pepe yangu?

Hapana. Tunazitumia kukuingiza na kulinda akaunti yako tu.

Ni lazima niwe na umri gani?

Miaka 13 au zaidi. Walio chini ya miaka 18 wanahitaji ruhusa ya mzazi au mlezi, na wanapiga soga kwa maneno yaliyoandaliwa tu.

Nafutaje akaunti yangu?

Ndani ya programu, au kwenye ukurasa wa akaunti yako hapa kwenye tovuti. drafti.co.tz/account

Drafti Ligi

Mechi zenye viwango · Kiswahili na English

Pakua Drafti Ligi